Pata Usaidizi Wetu:
Mtandaoni – Tunakuhimiza utumie Mchakato wetu mpya wa Kujiandikisha Mtandaoni. Utahitaji kufungua akaunti kwa kutumia jina lako na anwani sahihi ya barua pepe. Baada ya kufungua akaunti na kukamilisha mchakato wa kujiandikisha mtandaoni, mtu fulani atawasiliana nawe haraka iwezekanavyo ili kukupa maelezo au kuratibu miadi. Mchakato wetu wa kujiandikisha mtandaoni unapatikana kila wakati, lakini mtu fulani atafuatilia wakati wa saa za kawaida za kazi.
Saa za Kazi
-
Jumatatu saa 3:30 asubuhi hadi saa 12:00 jioni (9:30 a.m. – 5:30 p.m.)
- Jumanne saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni (8:00 a.m. – 6:00 p.m.)
- Jumatano saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni (8:00 a.m. – 6:00 p.m.)
- Alhamisi saa 3:30 asubuhi hadi saa 12:00 jioni (9:30 a.m. – 5:30 p.m.)
- Ijumaa: uandikishaji wa mtandaoni, faksi au barua pepe pekee
Kwa Simu – Ikiwa unapendelea kuzungumza na mtu ana kwa ana au unahitaji usaidizi wa kukamilisha mchakato wa kujiandikisha mtandaoni, tafadhali tupigie simu kwa nambari ya simu isiyolipishwa 1-866-297-2597 wakati wa saa zetu za kazi za Jumatatu hadi Ijumaa. Wafanyakazi wetu wanaweza kufikia huduma za ukalimani wa simu kwa zaidi ya lugha 150.
Kwa Faksi au kwa Barua – Pakua fomu ya Kuomba Huduma za Wapelelezi wa Malalamiko ya Wananchi (Ombuds) na uwasilishe fomu iliyojazwa kwa njia ya faksi, barua au barua pepe (maelezo ya mawasiliano yamechapishwa kwenye fomu) kwa OEO. Faksi: 1-844-886-5196
Wasiliana nasi kuhusu:
Swali au tatizo linalomwathiri mwanafunzi katika shule za umma za K-12 za Washington
Ombi la kupata mafunzo au uhamasishaji katika jamii, shule au mahali pako pa kazi