Pata Usaidizi Wetu:
Mtandaoni – Tunakuhimiza utumie Mchakato wetu mpya wa Kujiandikisha Mtandaoni. Utahitaji kufungua akaunti kwa kutumia jina lako na anwani sahihi ya barua pepe. Baada ya kufungua akaunti na kukamilisha mchakato wa kujiandikisha mtandaoni, mtu fulani atawasiliana nawe haraka iwezekanavyo ili kukupa maelezo au kuratibu miadi. Mchakato wetu wa kujiandikisha mtandaoni unapatikana kila wakati, lakini mtu fulani atafuatilia wakati wa saa za kawaida za kazi.
Saa za Kazi
-
Jumatatu saa 2:30 asubuhi hadi saa 11:00 jioni (8:30 a.m. – 5:00 p.m.)
-
Jumanne saa 2:30 asubuhi hadi saa 11:00 jioni (8:30 a.m. – 5:00 p.m.)
-
Jumatano saa 2:30 asubuhi hadi saa 11:00 jioni (8:30 a.m. – 5:00 p.m.)
-
Alhamisi saa 2:30 asubuhi hadi saa 11:00 jioni (8:30 a.m. – 5:00 p.m.)
-
Ijumaa saa 2:30 asubuhi hadi saa 11:00 jioni (8:30 a.m. – 5:00 p.m.)
Kwa Simu – Ikiwa unapendelea kuzungumza na mtu ana kwa ana au unahitaji usaidizi wa kukamilisha mchakato wa kujiandikisha mtandaoni, tafadhali tupigie simu kwa nambari ya simu isiyolipishwa 1-866-297-2597 wakati wa saa zetu za kazi za Jumatatu hadi Ijumaa. Wafanyakazi wetu wanaweza kufikia huduma za ukalimani wa simu kwa zaidi ya lugha 150.
Kwa Faksi au kwa Barua – Ili kuomba karatasi au fomu ya PDF, tuma barua pepe oeoinfo@gov.wa.gov
Kupata usaidizi kuhusu swali au tatizo lako:
Tafadhali tuwasiliane mtandaoni, au kwa simu, faksi, au barua. Tafadhali kumbuka kuwa ofisi ina wafanyikazi na ufadhili mdogo na inapeana kipaumbele kazi yake kulingana na vigezo vya mpango mkakati / Mpango wa Mikakati.
Utatuzi wa Migogoro Usio Rasmi
Office of the Education Ombuds (OEO) humsaidia mtu yeyote aliye na maswali au hoja kuhusu shule za umma za K-12 za Washington. Tunaweza kukupa maelezo, rufaa, zana na rasilimali nyingine.
Madhumuni ya kisheria ya Office of the Education Ombuds (OEO) ni kupunguza ukosefu wa fursa. Vipaumbele vya mpango wetu wa mikakati hulenga haki ya elimu, hasa kwa jamii zilizoathiriwa sana na COVID-19. Tunatumia rasilimali zetu ndogo za utatuzi wa migogoro, kama vile upatanishi na ukufunzi usio rasmi, kwa wanafunzi wa K-12 ambao:
- Hawapo shuleni, ikijumuisha wanafunzi wenye ulemavu wanaopokea huduma ya baadhi ya siku za shule
- Ni watu wa asili ya Kiafrika au wa makabila asili
- Hawana makao
- Wanatunzwa na jamaa au vituo vya makazi
- Wanashiriki katika masuala ya haki kwa vijana au mifumo ya kuwarekebisha vijana
- Ni wahamiaji rasmi au wasio rasmi, wakimbizi, watafutaji makazi rasmi au wanafunzi au familia ambazo lugha yao msingi si Kiingereza au
- Wanapokea usaidizi wa Mipango ya Wraparound yenye Huduma za Kina (Wraparound with Intensive Services, WISe) au Mipango ya Wagonjwa Wanaolazwa ya Muda Mrefu kwa Watoto (Children’s Long Term Inpatient Programs)
Tunaweza pia kuwafunza waelimishaji na watetezi wa jamii kuhusu kuwasaidia wanafunzi na kusuluhisha migogoro.
Tafadhali tuma barua pepe kwa oeoinfo@gov.wa.gov au piga simu kwa 1-866-297-2597 ili upate usaidizi huu. Mara nyingi, mmoja wa wahudumu wetu hujibu swali kwa barua pepe au kwa simu. Tunaruhusu mawasiliano kutoka kwa familia, wanafunzi, waelimishaji na wadau wengine wa jamii walio na maswali au matatizo.Ofisi yetu hufanya kazi kwa ushirikiano, kwa njia isiyo rasmi na kwa faragha, ili kuzisaidia familia na shule kusuluhisha migogoro.
