Uandikishaji Shuleni

Watoto wote wanaoishi kwenye Jimbo la Washington wanayo haki ya kupata elimu kwa umma.

Watoto wanaweza kujiunga kwenye shule ya chekechea wakiwa na umri wa miaka 5 na kuendelea na shule mpaka watakapohitimu au kufikisha umri wa miaka 21.

Inaanza kwa kujiandikisha (au kusajili). Maswali tunayoulizwa kuhusiana na kujiandikisha shuleni hujumuisha:

  • Ni taarifa au fomu gani zinazohitajika kwa ajili ya kujiandikisha?
  • Ni nani anayeweza kumwandikisha mwanafunzi?
  • Ni wapi ambapo mwanafunzi anaweza kujiandikisha, au ni shule gani inayoweza kuchaguliwa na familia?   

Bofya kwenye maswali yafuatayo.

Ni taarifa au fomu gani zinazohitajika kwa ajili ya kujiandikisha?

Ili kumwandikisha mwanafunzi shuleni, kwa ujumla shule huwa zinaomba hati kwa ajili ya:

  • Kuthibitisha anwani yako;
  • Kuthibitisha umri wa mtoto wako (hasa kwa ajili ya uandikishaji wa chekechea); na
  • Kuonyesha kwamba mwanao amepata chanjo zinazotakiwa.

Mara nyingi shule huorodhesha mifano ya aina za hati ambazo zinaweza kutumika katika uandikishaji. Iwapo huna hati maalumu zinazohitajika shuleni (mfano nakala ya bili, au cheti cha kuzaliwa cha mtoto wako), zungumza na ofisi ya uandikishaji ya shule kuhusu tatizo lako.

Mbadala wa Cheti cha Kuzaliwa/Hati ya Kusafiria: Shule lazima zikubali hati mbadala zinazoonyesha umri au tarehe ya kuzaliwa mtoto. Shule haiwezi kuendelea kung'ang'ania kupewa cheti cha kuzaliwa au hati ya kusafiria iwapo huna. Mbadala wake unaweza kuwa rekodi ya kuasili mtoto, nakala ya maelezo yaliyothibitishwa na daktari, au rekodi ya chanjo yenye tarehe ya kuzaliwa.

Uthibitisho wa Makazi: Shule mara nyingi huomba ushahidi wa eneo unaloishi ili kuwa na uhakika kwamba mwanao ni mkazi wa wilaya husika. Hata hivyo, ikiwa kwa sasa huna makazi ya kudumu (ikiwa huna nyumba), shule haiwezi kukataa kumwandikisha mwanao kama hutaweza kuwapatia hati. Ikiwa wewe au mwanao unayemtunza mnakabiliana na hili, omba msaada kwenye ofisi ya shule au wilaya ili uzungumze na “McKinney Vento Liaison (Msimamizi wa McKinney Vento).”

Kumbuka, watoto wote wanaoishi kwenye Jimbo la Washington wanayo haki ya kupata elimu ya umma. Ikiwa unajaribu kumwandikisha mwanao shuleni, lakini huna hati zinazotakiwa shuleni, tafadhali omba msaada.

Unaweza kuomba msaada shuleni au ofisi ya shule iliyopo wilayani. Unaweza kuwasiliana na ofisi zetu kupitia 1-866-297-2597 au kutembelea ukurasa Wetu wa Msaada ili kuwasiliana nasi kupitia kwenye mfumo wetu wa mtandaoni kwenye https://services.oeo.wa.gov/oeo 

Ni nani anayeweza kumwandikisha mwanafunzi?

Kwenye Jimbo la Washington, watu wanaoweza kuwaandikisha watoto wanajumuisha:

  • Wazazi au Walezi Halali
  • Mtu anayemwakilisha Mzazi iwapo mzazi au mlezi hayupo. Hii inaweza kujumuisha:
    • Ndugu anayetoa "Uangalizi wa Kidugu",
    • Wanaoishi na Mtoto kwa Muda, au
    • Mlezi anayemwakilisha mzazi.
  • Kijana Kujiandikisha Mwenyewe. Kijana asiyeishi na mzazi, na asiyekuwa na makazi ya kudumu au yanayofaa, anaweza kupata msaada wa kujiandikisha mwenyewe akiwa kama "Kijana Asiye na Makazi Aliye Peke Yake." Omba kuzungumza na McKinney Vento Liason ikiwa uko mwenyewe, au unamsaidia kijana ambaye yuko mwenyewe ili ajiandikishe shuleni.

Kwa mujibu wa Family Educational Rights and Privacy Act (FERPA, Sheria ya Haki na Faragha ya Elimu kwa Familia), sheria ya shirikisho inayohusiana na rekodi za elimu, "mzazi" anajumuisha mzazi halisi, mlezi, au mtu anayemwakilisha mzazi au mlezi asipokuwepo." (Unaweza kusoma zaidi kuhusu FERPA, kwenye tovuti ya (U.S. Department of Education (Idara ya Elimu ya Marekani): https://studentprivacy.ed.gov/.

Ikiwa mtoto anaishi kwenye makazi ya uangalizi kwa muda, kuna uwezekano wa kuwepo watu mbalimbali wanaoweza kutoa msaada wa kufanya maamuzi kuhusu elimu yake. Fomu ya Idhini ya Mlezi mara nyingi itaweka bayana mtu anayeweza kufanya maamuzi kuhusu elimu, ikijumuisha kumwandikisha mtoto shuleni. Kwa maelezo zaidi tazama Guide to Supporting Students in Foster Care (Mwongozo wa Msaada wa Wanafunzi Wanaolelewa kwa Muda), Unaopatikana kwenye Treehouse for Kids (www.treehouseforkids.org), kutoka kwenye Foster Care Program (Mpango wa Uangalizi wa Watoto kwa Muda) wa Office of Superintendent of Public Instruction (OSPI, Ofisi ya Msimamizi wa Mafunzo kwa Umma) (https://www.k12.wa.us/student-success/access-opportunity-education/foster-care), na kwenye hiki kiungo cha moja kwa moja: https://www.treehouseforkids.org/wp-content/uploads/2018/01/treehouse2017final2ndedinteractive.pdf

Ni wapi ambapo mwanafunzi anaweza kujiandikisha kujiunga na shule?  

Shule ya Wilaya ya Mkazi

Wanafunzi wote wanayo haki ya kupata elimu kwenye wilaya ambayo wanatumia muda wao mwingi kuishi. Hii ndiyo “shule ya wilaya ya mkazi” ya mwanafunzi. 

Makazi ya mwanafunzi yanaweza yasiwe sawa na yale ya wazazi wake.

Ufafanuzi wa Utawala wa Jimbo la Washington kuhusu makazi ya mwanafunzi unapatikana kwenye Washington Administrative Code (WAC, Kanuni ya Utawala wa Washingtoni), "WAC" kwenye WAC 392 - 137 - 115, ambayo unaweza kuipata mtandaoni kwenye: https://apps.leg.wa.gov/WAC/default.aspx?cite=392-137-115. Inafafanua kwamba makazi ya mwanafunzi ni pale ambapo mwanafunzi anatumia muda wake mwingi akiishi.

Upangaji wa Shule katika Wilaya

Kwa ujumla, kila shule ya wilaya inaweza kuamua namna ya kuwapanga wanafunzi katika shule mbalimbali ndani ya wilaya.

Shule nyingi za wilaya huwapanga wanafunzi kwenye shule zilizo karibu na eneo wanaloishi, mara nyingi hujulikana kama "eneo la mahudhurio" au shule ya jirani. Ikiwa shule ya jirani itazidiwa na idadi ya wanafunzi, shule za wilaya zinaweza kupanga wanafunzi kwenye shule nyinginezo zilizo ndani ya wilaya.

Shule za wilaya nyingi ambazo ni kubwa pia huwa na "usajili wa wazi" ambapo familia zinaweza kuomba usajili kwenye shule wanazopenda. Mara nyingi huwa ni mwanzoni mwa mwaka na kuendelea mpaka mwanzoni mwa masika. Unaweza kupata taarifa kutoka wilayani kwako kuhusiana na machaguo ya usajili wa shule.

Mara tu baada ya mwanafunzi kusajiliwa katika shule fulani, baadhi ya wilaya huruhusu uhamisho wa mwanafunzi iwapo tu kuna ugumu au sababu inayoshabihiana na hiyo. Shule nyingine hukubali uhamisho iwapo kuna nafasi. Omba sera na kanuni za wilaya yako ili kujifunza zaidi kuhusiana na machaguo yanayopatikana kwenye wilaya yako.

Kumbuka, kila mtoto anayo haki ya kupata elimu kwenye shule ya wilaya anayoishi. Ikiwa unakabiliwa na vizingiti vya uandikishaji, unaweza kuwasiliana na ofisi yetu kupitia 1-866-297-2597 au kwa barua pepe kwenye, au kupitia mfumo wetu wa mtandaoni kwenye: https://services.oeo.wa.gov/oeo

Shule ya Origin - Makazi ya Muda au Hana Makazi

Watoto wasiokuwa na makazi au wanaoishi kwenye makazi ya muda wanaweza kuhudhuria shule kwenye eneo wanaloishi kwa wakati huo, au, wanaweza kupata msaada wa kubaki kwenye "Shule Yao ya Origin," hata kama walipaswa kuhamia kwenye eneo tofauti. 

Sheria inayowalinda na kuwasaidia wanafunzi ambao hawana makazi inaitwa “McKinney Vento Act (Sheria ya McKinney Vento)”, na kila shule ya wilaya yupo McKinney Vento Liaison (Msimamizi wa McKinney Vento) ili kusaidia familia na wanafunzi wasiokuwa na makazi. Hii inajumuisha wanafunzi na familia zinazoishi kwa marafiki au ndugu kwa sababu hazina makazi binafsi. Ikiwa wewe au mwanao anastahiki kupata msaada wa McKinney Vento, ikiwemo kubaki kwenye Shule yake ya Origin, tafadhali omba kuzungumza na “McKinney Vento Liaison” wa wilaya. Unaweza kupata taarifa zaidi kuhusiana na Msaada kwa Wanafunzi Wasiokuwa na Mkazi kwenye tovuti yetu.

Sheria ya shirikisho ya elimu inayojulikana kama "ESSA," (the Every Student Succeeds Act, Sheria ya Mafanikio ya Kila Mwanafunzi), imeongeza kipengele ili kuipatia shule ya mwanzo, usafiri na kinga kwa ajili ya uandikishaji wa haraka kwa wanafunzi wanaoishi kwenye makazi ya uangalizi wa muda. Ikiwa unamtunza mtoto kwenye makazi ya muda, omba kuzungumza na “Foster Care Liaison” (Msimamizi wa Makazi ya Muda) ili kuona ni kwa jinsi gani wanaweza kukusaidia katika elimu ya mtoto wako.

Soma zaidi kuhusiana na kinga na msaada kwa wanafunzi wanaoishi kwenye Makazi ya Muda kupitia Guide to Supporting Students in Foster Care (Mwongozo wa Kuwasaidia Wanafunzi Wanaoishi kwenye Uangalizi wa Muda Mfupi), Unaopatikana kwenye Treehouse for Kids (https://www.treehouseforkids.org/), kutoka kwenye OSPI’s Foster Care Program (Mpango wa Uangalizi wa Watoto kwa Muda) (https://www.k12.wa.us/student-success/access-opportunity-education/foster-care), na kwenye kiungo hiki cha moja kwa moja: https://www.treehouseforkids.org/wp-content/uploads/2018/01/treehouse2017final2ndedinteractive.pdf

Machaguo ya Uchaguzi wa Shule na Uhamisho Kwenda Wilaya Nyingine     

Kuna aina nyingi za machaguo ya shule za umma kwenye Jimbo letu. Ikiwa unataka kuchunguza chaguo ambalo halipatikani kwenye wilaya yako lakini linapatikana kwenye wilaya ya karibu au mtandaoni, unaweza kuomba kuzungumza na wilaya kuhusiana na “uhamisho kwa asiyekuwa mkazi”—ikimaanisha, unapendelea mwanafunzi wako apate huduma zilizo nje ya wilaya yako.   

Kila wilaya lazima iwe na sera inayohusiana na uhamisho wa “wale wasiokuwa wakazi” au "uchaguzi". Uombaji wa uhamisho kutoka wilaya moja kwenda nyingine ni mchakato unaojumuisha hatua mbili, unaohitaji wilaya anayoishi mkazi kuachilia mwanafunzi na wilaya asiyoishi mwanafunzi kumkubali. Unaweza kupata kiungo cha ombi la uchaguzi wa uhamisho kwenye tovuti ya OSPI kwenye: https://www.k12.wa.us/student-success/support-programs/student-transfers au kwa kuomba kwenye wilaya yako. Tembelea ukurasa wetu wa Chaguo la Shule / UhamishoSeti ya Zana za Uchaguzi wa Uhamisho na tovuti ya OSPI ya Uhamisho wa Mwanafunzi ili kupata taarifa zaidi.

Baadhi ya machaguo ya shule za umma ndani ya Jimbo la Wasington yanajumuisha:

Uzoefu Mbadala wa Kujifunza, unaojumuisha Mtandao na Ushirika wa Nyumbani/Shuleni:

Baadhi ya shule za wilaya hutoa "Njia Mbadala ya Uzoefu wa Kujifunza," aina ya elimu kwa umma ambapo maelezo baadhi au yote hutolewa nje ya mfumo wa kawaida wa darasani. Hii inajumuisha shule za mtandao, na mipango ya ushirika wa nyumbani/shuleni.   

Uliza kwenye ofisi ya shule ya wilaya yako, au tembelea tovuti ya wilaya yako kupata taarifa inayohusiana na machaguo mbadara kwenye eneo lako.

Unaweza pia kupata orodha ya Mipango Mbadara ya Mafunzo ya OSPI ya Shule Mtandaoni iliyopitishwa kwa kutembelea kurasa za tovuti, hapa: https://ospi.k12.wa.us/student-success/career-technical-education-cte/cte-skill-centers.

Vituo vya Ujuzi vya Kikanda:

Vituo vya Ujuzi ni mipango ya kikanda inayotoa kozi mbalimbali katika taaluma na ufundi kwa wanafunzi wa shule ya upili. Kuna zaidi ya vituo vya ujuzi kumi na viwili, na matawi kadhaa ya vyuo hivi katika maeneo tofauti jimboni. Unaweza kuomba taarifa kutoka kwa mshauri wako wa shule ya upili au kutoka kwenye ofisi ya wilaya ili kuona iwapo wilaya yako inashiriki kwenye mpango wa Vituo vya Ujuzi, na kozi ambazo zinatolewa.

Pia unaweza kuona orodha kamili ya Vituo vya Ujuzi, na viungo vya tovuti zake, kupitia ukurasa wa OSPI wa kazi na elimu ya ufundi, hapa: https://ospi.k12.wa.us/student-success/career-technical-education-cte/cte-skill-centers.

Mipango ya Open Doors Re-Engagement:

Wilaya nyingi zimeunda mipango ya Open Doors Youth Reengagement (Mipango ya Wazi ya Ushiriki Tena kwa Vijana) ambayo inasaidia wanafunzi wenye umri wa miaka 16-21 waliopoteza mwelekeo wa shule, lakini wangependa kujaribu tena. Mipango Open Doors mara nyingi inakuwa na ratiba zinazoweza kubadilika, na hufanya kazi kwa ukaribu na vijana ili kutengeneza mwelekeo wa kuhitimu na mafanikio.  Ikiwa kama unatafuta njia mbadara ya kurudi shuleni, au kurudi kwenye mwelekeo, muombe mshauri wa shule ya upili au mtu yeyote aliyeko kwenye ofisi ya wilaya akueleze kama kuna mpango wa Re-engagement (Ushiriki tena katika eneo lililo karibu nawe.

Unaweza pia kuwasiliana nasi ili uone kama tunaweza kukupatia msaada wa machaguo. Unaweza kuwasiliana nasi kupitia 1-866-297-2597, au tutumie barua pepe kupitia oeoinfo@gov.wa.gov, au ungana nasi kupitia mfumo wetu wa usajili kwenye: https://services.oeo.wa.gov/oeo.

Machaguo Mengeneyo ya Shule za Umma

Ukiachana na shule zinazoendeshwa na shule za wilaya 295 katika jimbo la Washington, machaguo ya shule za umma katika Jimbo la Washington pia hujumuisha:

  • State School for the Blind, na
  • State School for the Deaf;
  • Shule za kikabila, na
  • Shule za Umma za Kukodisha.

Unaweza kupata taarifa kuhusiana na shule za Kikabila kwenye tovuti ya Office of Native Education (Ofisi ya Elimu Asilia ya OSPI) kwenye tovuti ya: https://www.k12.wa.us/student-success/access-opportunity-education/native-education/types-tribal-schools.

Unaweza kupata taarifa mtandaoni kuhusiana na shule za umma za kukodisha zinazofanya kazi kutoka kwenye Washington Charter School Commission (Tume ya Shule za Umma za Kukodisha Jimboni Washington), kupitia: https://charterschool.wa.gov/. Kwa orodha ya shule za umma za kukodisha zilizoidhinishwa na Tume, na ambazo zinafanya kazi kwa sasa, pitia hapa: https://charterschool.wa.gov/our-charter-public-schools/

Kwa shule za umma za kukodisha zilizoidhinishwa na Spokane Public Schools (Shule za Umma za Spokane), tembelea hapa:https://www.spokaneschools.org/page/charter-school-authorization

Tembelea kurasa zetu za Seti ya Zana za Uchaguzi wa Shule / Uhamisho na tovuti ya OSPI ya Uhamisho wa Mwanafunzi, https://www.k12.wa.us/student-success/support-programs/student-transfers, ili kupata maelezo zaidi.