VIDOKEZO & ZANA KWA FAMILIA: Kushughulikia Ubaguzi Shuleni
Ubaguzi ni utendaji usio wa haki au usawa au unyanyasaji wa mtu kwasababu yeye ni sehemu ya kikundi kinachojulikana kama tabaka linalolindwa. Tabaka linalolindwa linajumuisha watu ambao wana sifa zinazofanana na wanalindwa na sheria dhidi ya ubaguzi na unyanyasaji.[1]
[1] Ofisi ya Usawa na Haki za Kiraia, Ofisi ya Msimamizi wa Mafunzo ya Umma. Ubaguzi, Unyanyasaji wa Ubaguzi, na Unyanyasaji wa Kingono: Utatuzi wa Mizozo. Imetolewa kutoka: https://ospi.k12.wa.us/policy-funding/equity-and-civil-rights
Unyanyasaji wa kibaguzi:
Hutokea dhidi ya tabaka linalolindwa +
Una uwezo mkubwa wa kutengeneza mazingira magumu
Matabaka Yanayolindwa chini ya Sheria ya Jimbo la Washington ni:
- Asili na Rangi
- Asili ya Utaifa
- Dini na Imani
- Jinsia
- Utambulisho wa Jinsia
- Maonyesho ya Jinsia
- Mwelekeo wa Kimapenzi
- Ukongwe wa kijeshi au Hadhi ya Kijeshi
- Ulemavu
- Matumizi ya Huduma ya Wanyama
Unyanyasaji wa kibaguzi hauhitaji kuelekezwa kwa mtu maalumu na unaweza kuwa:
- Vitisho
- Kuita majina yasiyofaa
- Utani wa dharau
- Shambulio la kimwili
- Tabia zingine za vitisho vya kimwili, kuumiza, au
[1] Angalia juu
Mazingira magumu hutokea pindi unyanyasaji wa ubaguzi unapokuwa mkubwa, kuenea, au kuimarika kiasi cha kuingilia uwezo wa mwanafunzi kushiriki au kufaidika na huduma, shughuli, au fursa ambazo shule au wilaya imetoa. Wanafunzi wanaopitia mazingira magumu wanaweza kuonekana kuwa na huzuni au hasira, wagonjwa kushinda hali yao ya kawaida, kupata alama za chini, au kuepuka shule.
Je, ni lini wilaya ya shule itawajibika?
Wilaya lazima ichukue hatua za kushughulikia unyanyasaji wa kibaguzi pindi inapojua au kupaswa kujua unatokea. Ikiwa unafanyika darasani, ukumbini, mapumzikoni au kwenye basi na kushuhudiwa na wafanyakazi wa shule, wafanyakazi hao wanapaswa kutoa taarifa kwa mkuu wa shule ili shule iweze kushughulikia kwa ufanisi.
Wilaya lazima pia zirekebishe sera zao zozote zinazoweza kuwa na athari isiyotarajiwa ya ubaguzi kwa mwanafunzi au kikundi cha wanafunzi kulingana na tabaka lao linalolindwa.
Je, nitajuaje kama ni ubaguzi au ni kitu kingine?
Unaweza kuona ni vigumu kujua ikiwa tatizo ambalo mtoto wako anapitia ni kwa sababu ya ubaguzi au kitu kingine. Ikiwa mtoto wako ataangukia katika mojawapo ya matabaka yaliyolindwa, amepitia mazingira magumu, na shule haijashughulikia suala hilo, fikiria maswali haya:
- Kwa nini nadhani tatizo hili linatokea?
- Kwa nini mtoto wangu anadhani tatizo hili linatokea?
- Kwa nini mwalimu wa mtoto wangu anadhani tatizo hili linatokea?
- Tatizo hili limetokea kwa mtu mwingine? Kwa nini?
Ikiwa mtoto wako anabaguliwa, shirikisha jambo hilo na wilaya ili wafanyakazi waweze kuchunguza na kulishughulikia ipasavyo.
Mambo ya Kufikiria Kabla ya Kukutana na Shule au Wilaya
- Andika kila kitu ambacho wewe au mtoto wako anaweza kumbuka kuhusu (ma)tukio, kama vile tarehe, saa na watu wanaohusika. Leta maelezo yako kwa maandishi kwenye kikao na shule au wilaya.
- Fikiria kile mtoto wako anahitaji na kile shule inahitaji kufanya ili kutatua hali hii. Fikiria kuhusu:
- Ni mabadiliko gani yanahitajika kutokea ili kushughulikia hali ya shule au utamaduni wake ili tabia hii isijirudie kwa mtoto wako au mwanafunzi mwingine?
- Je, ni usaidizi gani ambao wafanyakazi na/au wanafunzi wengine wanaweza kuhitaji ili kufanya shule iwe yenye kumkaribisha kila mtu?
- Mtoto wako anahitaji nini ili kujisikia salama na kutulia shuleni? Fikiria jinsi ya kushughulikia sio tu tukio la mtu binafsi, lakini pia hali ya shule au utamaduni. Zana moja inaweza kuwa mpango wa usalama wa kuhakikisha kuwa wanyanyasaji wanaoshutumiwa hawatakuwa katika darasa moja au eneo moja.
- Adhabu ya mtu husika kwa wanafunzi inaweza kufaa, lakini mara nyingi hatua ya aina hii haitamaliza mazingira magumu au kuzuia unyanyasaji kutokea tena.
Angalia: Ofisi ya Msimamizi wa Mafunzo ya Umma, Usawa na Haki za Kiraia. Malalamiko na Mashtaka kuhusu Ubaguzi: https://ospi.k12.wa.us/policy-funding/equity-and-civil-rights/complaints-and-concerns-about-discrimination. Hatua zinazofuata |
njia za kuwasilisha malalamiko rasmi
Wilaya za Shule
- Unaweza kuwasilisha malalamiko moja kwa moja kwa wilaya ya shule kupitia mkuu wa shule au mratibu wa haki za kiraia wa wilaya. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya wilaya ya shule yako.
Ofisi ya Jimbo la Washington ya Msimamizi wa Ofisi ya Mafunzo ya Umma ya Usawa na Haki za Kiraia
- Ofisi ya OSPI ya Usawa na Haki za Kiraia itazingatia malalamiko kuhusu ubaguzi, unyanyasaji wa kibaguzi, na unyanyasaji wa kingono pindi tu machaguzi ya malalamiko ya wilaya ya shule yatakapofuatiliwa. Kwa taarifa zaidi: https://ospi.k12.wa.us/policy-funding/equity-and-civil-rights/complaints-and-concerns-about-discrimination
Ofisi ya Idara ya Elimu ya Marekani ya Haki za Kiraia (OCR)
- OCR inatekeleza haki za kiraia za shirikisho zinazokataza ubaguzi katika programu au shughuli kulingana na asili, rangi, asili ya kitaifa, jinsia, ulemavu na umri. Kwa taarifa zaidi: https://www.ed.gov/about/ed-offices/ocr
Tume ya Haki za Kibinadamu ya Jimbo la Washington
- WSHRC inatekeleza Sheria ya Washington dhidi ya Ubaguzi (RCW 49.60), ambayo inakataza ubaguzi kwenye ajira na katika maeneo ya makazi ya umma, yakiwemo shule. Kwa taarifa zaidi: https://www.hum.wa.gov/file-complaint
Idara ya Haki ya MarekanI (DOJ), Sehemu ya Fursa za Elimu
- DOJ hutekeleza sheria za shirikisho za haki za kiraia ambazo zinakataza ubaguzi kwa misingi ya asili, rangi, asili ya kitaifa, jinsia, ulemavu na dini katika shule za umma. Kwa taarifa zaidi: https://www.justice.gov/crt/educational-opportunities-section
Malalamiko kwa undani: Wakala na Sheria/Sera zinazotekelezwa |
Malalamiko yaliyoandikwa yanahitajika? |
Muda wa kuwasilisha Malalamiko |
Muda wa Kukamilisha Upelelezi/Uamuzi wa Wakala |
Wilaya ya Shule
Sera na utaratibu dhidi ya ubaguzi.[1]
|
Ndiyo[2] |
Tazama sera; Sio chini ya mwaka 1.
Siku 10 za kalenda kukata rufaa kwa bodi ya shule (au siku 30 za kalenda ikiwa hakuna jibu kutoka kwa Msimamizi) |
Ndani ya siku 30 za kalenda baada ya malalamiko: Jibu la maandishi kutoka kwa Msimamizi.
Kama ikikatwa rufaa kwa bodi ya shule: Kusikiza ndani ya siku 20 za kalenda na maamuzi kwa maandishi ndani ya siku 10 za kalenda na maelezo yaliyotolewa kuhusu chaguo la kukata rufaa kwa OSPI. |
OSPI – Usawa & Haki za Kiraia[3]
RCW 28A.642.010
WAC 392-190
|
Ndiyo |
Ndani ya siku 20 za kalenda baada ya kupokea uamuzi wa bodi ya shule, isipokuwa muda ukiongezwa na OSPI kwa sababu nzuri |
OSPI "inaweza kuanzisha uchunguzi"; Hakuna muda maalumu wa kukamilisha uchunguzi. Baada ya uchunguzi, OSPI itatoa uamuzi kwa maandishi.
|
Tume ya Haki za Kibinadamu ya Jimbo la Washington (WSHRC)[4]
Sheria ya Washington dhidi ya Ubaguzi RCW 49.60 |
Ndiyo |
Ndani ya miezi 6 tangu tarehe ya madai ya ubaguzi |
Wasiliana na WSHRC kwa maelezo zaidi kuhusu mchakato wao wa malalamiko ya ubaguzi wa makazi ya umma. |
Idara ya Elimu ya Marekani Ofisi ya Haki za Kiraia (OCR)[5]
|
NDIYO |
Kwa ujumla ndani ya siku 180 za kalenda baada ya madai ya ubaguzi isipokuwa muda umeongezwa na OCR kwa sababu nzuri iliyoonyeshwa |
OCR inachunguza malalamiko “kwa wakati unaofaa” na itawajulisha walalamikaji kuhusu uchunguzi. Mwishoni mwa uchunguzi, OCR hutoa matokeo kwa maandishi. |
Idara ya Haki ya Marekani (DOJ)[6]
|
Ndiyo |
Hapana |
Hakuna kikomo cha muda mahususi. |
[1] WAC 392-190 (Wilaya za shule lazima zichukue na kutekeleza taratibu za malalamiko na rufaa ili kuchunguza na kutatua madai ya ubaguzi na unyanyasaji wa kibaguzi.)
[2] Wilaya pia zinaweza kupitisha utaratibu usio rasmi wa malalamiko ila wakati wa kutumia utaratibu huo usio rasmi, lazima wawajulishe walalamikaji kuwa wana haki ya kuwasilisha malalamiko rasmi. WAC 392-190-065.
[4] Tume ya Haki za Binadamu https://www.hum.wa.gov/file-complaint
[6] Sehemu ya Fursa za Kielimu https://www.justice.gov/crt/educational-opportunities-section