Elimu Maalum ya Utatuzi wa Mgogoro
Iliyosasishwa Juni 2024
Nahitajika kufanya nini ili kutatua mgogoro na shule ya wilaya?
Kutana na wilaya, omba upatanisho, lalamika ama tuma ombi la kusikilizwa kwa utaratibu wa haki.
Huku unapopigania mwanafunzi wako mwenye ulemavu, unaweza kujikuta kutokubaliana na wilaya ya shule. Kila itakapowekezana, ni wazi zuri kujaribu kutatua tatizo kwa kuzungumza na wanachama wa Individual Education Program (IEP, Timu ya Programu ya Elimu Binafsi) ama wahusika wengine wa wilaya ya shule. Ikiwa utaratibu huo hautafanya kazi, kuna njia mbali mbali za kutatua migogoro zilizopo kwenye sheria.
Taratibu rasmi za malalamiko, upatanisho, utaratibu mzuri wa kusikiliza malalamiko unapatikana kwa wazazi na shule ili kutatua migogoro kuhusu elimu maalum, ikiwa ni pamoja na kutoelewana kuhusu:
- Utambulisho wa mwanafunzi kama mlemavu
- Kupandishwa daraja kwa mwanafunzi
- Utoaji wa huduma maalum ya elimu
- Kuandikishwa kielimu kwa mtoto.
Malalamishi
Kuna mifumo miwili rasmi iliyopo ya kutoa malalamishi iwapo kuna hali ya kutoelewana kuhusu programu ya elimu maalum ya Individuals with Disabilities Education Act –(IDEA, Sheria ya Elimu ya Watu Wanaoishi na Ulemavu) (IDEA ama 504) kwa mwanafunzi.
- Malalamiko ya Jamii ya Elimu Maalum kwa Jimbo la Washington State, Office of the Suprintendent of Public Instruction.
Je, Malalamiko ya Jamii ya Elimu Maalum ni nini? ni nini?
Malalamiko ya Jamii ya Elimu Maalum, iliyofahamika awali kama Malalamiko ya Mwananchi, ni njia ya kuwa na kutoelewana baina ya wanafunzi na wilaya kutatuliwa na wakala wa nje. Malalamiko ya jamii yanafaa kufikishwa kwa Office of the Superintendent of Public Instruction (OSPI, Ofisi ya Msimamizi wa Mafunzo ya Umma) wakati mtu anapoamini kwamba kituo cha elimu (ikiwa ni pamoja na shule ya jimbo, wilaya ya shule, ama umma ama binafsi) kimekiuka mahitaji ya (Individuals with Disabilities Education Act –IDEA) Sheria ya Elimu ya Watu Wanaoishi na Ulemavu ama masharti ya jimbo ya elimu maalum.
Je, ni nani anayeweza kutuma malalamiko kuhusu Jamii ya Elimu Maalum?
Mtu ama Shirika lolote linaweza kisajili malalamiko katika ofisi ya Office of the Superintendent of Public Instruction.
Je, ni yapi mahitaji ya Malalamiko kuhusu Jamii ya Elimu Maalum?
Malalamiko lazima yawe:
- Kwa maandishi
- Yatiwe sahihi na mlalamishi
- Ikiwa ni pamoja na taarifa ambayo kituo hicho cha elimu kimekiuka sheria za elimu maalum kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita
- Kueleza bayana kuhusu ukiukaji huo
- Orodhesha jina na anwani ya mlalamishi, na
- Orodhesha jina na anwani ya kituo cha kielimu.
Iwapo malalamishi hayo yanahusu mwanafunzi maalum, basi malalamiko hayo yanapaswa kuwa na:
-
- Jina la mwanafunzi
- Jina la wilaya ya shule ya mwanafunzi
- Maelezo ya tatizo linaloathiri mwanafunzi
- Suluhu iliyopendekezwa kuhusu tatizo hilo.
Je, ni wapi mahali inapopatikana fomu ya Malalamishi ya Jamii?
OSPI imeunda fomu m’badala kwa ajili matumizi yako wakati wa kujaza malalamiko ya Jamii ya elimu Maalum. Fomu hii inapatikana katika: https://ospi.k12.wa.us/student-success/special-education/dispute-resolution/file-community-complaint
Ni wapi unaweza kuathiri pakubwa?
Unapotia malalamiko ya jamii, hakikisha kutazama nyakati kwa makini. Iwapo OSPI ama kituo cha kielimu hakitachukua hatua ndani ya muda uliowekwa, una fursa ya kulalamika tena.
Hakikisha kwamba umeonyesha rekodi mahususi ya shule ikiwa na kurasa zenye nambari zilizo na malalamishi ili pawe na urahisi wa kurejelea kurasa hizo.
Je, itakuwaje baada ya kujaza malalamiko ya Jamii ya Elimu Maalum?
Pindi tu OSPI wakipokea malalamishi, ni lazima itume nakala ya malalamishi hayo kwa wilaya ya shule. Ndani ya siku 20 baada ya kupokea malalamishi, wilaya ya shule lazima ichunguze malalamishi na kujibu kwa maandiko kwa OSPI. OSPI watakutumia nakala ya majibu ya wilaya ya shule. Basi una chaguo la kutuma taarifa ya ziada kuhusu malalamishi.
Ndani ya siku 60, OSPI lazima ifanye maamuzi huru na kwa maandiko ili kujua iwapo kituo hicho cha elimu kinavunja sheria maalum ya elimu ya shirikisho ama jimbo. Maamuzi lazima yahusishe matokeo ya ukweli na hatua muhimu ili kutatua malalamiko. Muda unaweza kuongezewa iwapo:
1) kuna hali ya kipekee inayohusiana na malalamiko ama
2) mlalamishi na kituo cha elimu kitakubali kwa maandiko kuongezea muda wa kutumia upatanisho au mbinu ya utatuzi wa mgogoro mwingine.
Hivyo basi, Wilaya ya shule ni lazima izingatie nyakati zilizowekwa katika maamuzi yaliyoandikwa ya OSPI ili kukamilisha hatua yoyote ya marekebisho iliyopendekezwa. Iwapo wilaya ya shule haitakuwa na ufuatiliaji, OSPI inaweza kuzuia ufadhili kwa wilaya ama kuamrisha kutumika kwa mbinu nyinginezo za kupata suluhu.
Iwapo imeamuliwa kwamba wilaya ya shule haikutoa huduma zinazostahili kwa mwanafunzi aliye na ulemavu, basi OSPI ni lazima:
- Iamue jinsi ambavyo wilaya ya shule itakavyofidia kukosekana huko kwa huduma, ikiwa ni pamoja na kulipa pesa ama kuchukua hatua nyingine za marekebisho ili kushughulikia mahitaji ya mwanafunzi.
- Shughulikia utoaji wa huduma katika siku za baadae kwa wanafunzi wote walio na ulemavu.
Je, ni wapi nitapata taarifa zaidi kuhusu Malalamishi ya Jamii ya OSPI?
https://ospi.k12.wa.us/student-success/special-education/dispute-resolution/file-community-complaint
Malalamishi ya Haki za Raia kwa Marekani katika Office of Civil Rights for the Department of Education
Je, Malalamishi ya Haki za Raia ni nini?
Kifungu cha 504 ni sheria dhidi ya ubaguzi kinacholenga kumaliza ubaguzi unaohusiana na ulemavu katika programu zote zinazopokea ufadhili kutoka kwa shirikisho. Kwa kuwa shule za umma na zile za wilaya hupokea fedha za shirikisho, basi zinashirikishwa kwenye mahitaji ya kifungu cha 504.
Office for Civil Rights (OCR, Ofisi ya Marekani ya Haki za Raia) kwa Department of Education (Idara ya Elimu ya Marekani) hushughulikia kikamilifu ulinzi wa Kifungu cha 504 na inawajibikia malalamishi yanayohusu uchunguzi.
Ni nani anayeweza kutoa malalamishi ya haki za raia?
Mtu yoyote anaweza kutoa malalamishi katika Office of Civil Rights nchini Marekani, kila wakati mwanafunzi aliye na ulemavu anapokosa kupokea manufaa ya kielimu kutoka kwa programu ambayo inalinganishwa na manufaa yaliyopatikana kwa wenzao ambao sio walemavu. Mfano ni pale ambapo mwanafunzi mwenye hulka ya ulemavu anapoambiwa kwamba hawezi kwenye safari za nyanjani na ni lazima abakie kwenye ofisi ya Mwalimu Mkuu huku wengine wote darasani wanapoondoka kwenda nyanjani. Malalamishi ya OCR yanaweza kuhusisha tatizo la ufikiaji, kama vile kukosekana kwa tuta la mtoto mwenye kiti cha magurudumu ama wilaya kutotoa malazi au huduma zinazofaa ama ziwe kwenye mpango wa mwanafunzi wa 504.
Ni yapi mahitaji ya malalamishi ya haki za raia?
Malalamishi ya haki ya raia lazima itolewe ndani ya siku 180 (miezi 6) za tarehe ya ubaguzi. Malalamishi hayo yanafaa kuhusisha:
► Jina, anwani na nambari ya simu ya anayejaza
► Jina, anwani na nambari ya simu ya watu waliobaguliwa
► Jina, anwani ya shule, wilaya, ama mtu aliyebaguliwa
► Msingi wa ubaguzi (ukoo, ulemavu, uhalisia wa kitaifa, nk.)
► Lini na wapi ambapo ubaguzi huo ulifanyika
► Ukweli kuhusu ubaguzi huo na
► Nakala ya nyaraka iliyoandikwa, data, ama nyaraka nyinginezo zinazounga mkono malalamishi.
Ni wapi pa kupeleka malalamishi ya OCR ya Haki ya Raia?
Ili kuandikisha malalamishi kupitia kwa OCR, unaweza kutumia fomu ya malalamishi ya kiektroniki inayopatikana kwenye: https://www2.ed.gov/about/offices/list/ocr/complaintintro.html
ama kamilisha fomu inayojazika kwa wepesi kupitia: https://www2.ed.gov/about/offices/list/ocr/complaintform.pdf
Iwapo utachagua kukamilisha fomu hiyo ama kuandika barua yako kivyako, unaweza kutuma malalamishi kupitia kwa baruapepe OCR.Seattle@ed.gov ama kupitia kwa kipepesi kwa (206) 607-1601 Unaweza pia kutuma malalamishi yako kupitia kwa baruapepe ya:
Office for Civil Rights
U.S. Department of Education
915 2nd Avenue #3310
Seattle, WA 981074-1099.
Je, itakuwaje baada ya kutuma malalamishi kuhusu haki za raia?
Taarifa ya uhakiki wa OCR katika malalamishi na kuamua iwapo ama malalamishi hayo hayatashughulikiwa tena. Ni lazima iamuliwe iwapo itakuwa na mamlaka ya kuchunguza malalamishi na iwapo malalamishi hayo yametumwa kwa muda na utaratibu unaostahili. Malalamishi lazima yajazwe ndani ya siku 180 kufuatia tarehe ya madai ya kitendo hicho cha ubaguzi.
OCR itakuuliza kutia sahihi fomu ya ukubalifu kama sehemu ya utaratibu huu. OCR itawasiliana nawe kupitia kwa njia ya baruapepe ama simu iwapo fomu hii haitakuwa imepokelewa kufikia siku ya 15 kutokea wakati ulipoulizwa kutia sahihi na kukufahamisha kwamba una siku 5 zaidi za kutia sahihi fomu hiyo. Kadhalika, unaweza kuulizwa ili kutoa taarifa ya ziada. Iwapo taarifa zaidi itahitajika, lazima OCR ikupatie angalau siku 20 ili kutoa taarifa inayohitajika.
Baada ya OCR kukamilisha uchunguzi wake, wewe na wilaya mtapokea Barua ya Uchunguzi ambayo itafafanua iwapo ushahidi unaunga mkono kama ukiukaji huo ulitokea. Iwapo OCR itagundua kwamba wilaya haikufuata sheria, itawasiliana na wilaya ili kujua iwapo wilaya iko tayari kuingia kwenye makubaliano ya hiari ya kutafuta suluhu. Iwapo wilaya haitakubali kutatua tatizo hili, OCR inaweza kuchukua hatua zaidi kama vile kuituma kesi hiyo kwa Idara ya Haki.
Iwapo unahisi wilaya inakiuka haki ya mwanafunzi ya kupata elimu inayofaa, iamue kuweka malalamishi.
Upatanisho
Upatanisho ni nini?
Upatanisho ni aina ya utatuzi wa migogoro. Chini ya IDEA, majimbo yanahitajika kutoa huduma za upatanisho bila malipo kwa wazazi/walezi na wilaya za shule kwa ajili ya kusuluhisha migogoro kuhusu programu maalum ya elimu kwa mwanafunzi.
Utaratibu wa upatanisho inaleta shule na mzazi au mlezi, pamoja mtu mwingine ambaye haegemei upande wowote – mpatanishi. Mpatanishi huyo atakutana nao wote ili kujaribu kuwapatanisha katika mahitaji ya elimu ya mwanafunzi. Mchakato huu ni wa hiari, kwa hivyo mzazi ama mlezi na wilaya ya shule itabidi wakubali ili kushiriki. Upatanishi utakuwa njia muafaka ya huduma ya kuimarisha kwa mwanafunzi, tatua matatizo, na rekebisha mahusiano kati ya shule na mzazi au mlezi.
Iwapo upatanisho utafaulu, pande zote mbili zitatia sahihi makubaliano ya kisheria yanayoelezea kuhusu mapatano hayo. Ni kwa maamuzi ya shule na mzazi ama mlezi ili kufanya kanuni za maagano hayo. Pindi tu makubaliano yatafanywa, mpatanishi atajiondoa na hakutakuwa na ulazimishaji wa upande wowote katika kulazimishwa kufanya chochote. Iwapo mgogoro utatokea wakati wa makubaliano ya upatanishi, mzazi ama mlezi inaweza kutaka makubaliano hayo kuidhinishwa na korti au shirikisho. Iwapo mgogoro mpya mpya au tofauti utaibuka, mzazi au mlezi ama wilaya inaweza kutumia mbinu zote za usuluhishaji wa migogoro inayopatikana kwenye sheria.
Ombi la upatanishi linafaa kutolewa kwa Machaguo Muhimu. Unaweza kutuma ombi kwa maandishi au kwa njia ya simu. Pande zote zinaweza kuwasiliana na Machagua Muhimu na watawasiliana na wahusika wengine. Unaweza kufikia Machaguo Muhimu kupitia kwa 1-800-692-2540.
Dokezo la Mazungumzo
Kukubali kushiriki katika upatanishi hakukuzuii wewe kuuliza malalamishi yako kusikilizwa baadae. Unaweza kusitisha mchakato wa upatanishi wakati wowote na bado kuuliza kuhusu mchakato wa kusikilizwa kwa malalamishi. Pingamizi moja ni kwamba usikilizwaji wa baadae, mazungumzo yaliyofanyika wakati wa mchakato wa upatanishi, hauwezi kutumika kama ushahidi. Hata hivyo, makubaliano ya upatanishi yaliyoandikwa yanaweza kutumika kama ushahidi.
Mchakato wa Usikilizwaji wa Malalamishi
Mchakato wa Usikilizwaji wa Malalamishi ni nini?
Mchakato wa Usuluhishaji wa Malalamishi ni utaratibu rasmi wa kiusimamizi, kama vile jaribio. Mzazi au mlezi na wilaya ya shule ambaye ana fursa ya kutoa ushahidi na mashahidi na kuwahoji mashahidi na upande mwingine.
Ofisa wa usuluhishaji ataandika maamuzi kuambatana na ukweli pamoja na sheria.
Je, ninahitaji wakili katika mchakato huu wa kusikilizwa kwa malalamishi?
Hapana, lakini una haki ya kuwakilishwa na wakili iwapo ungependa.
Mzazi ama mlezi wa mwanafunzi mwenye ulemavu anaweza kushauriwa ama kuwakilishwa na wakili katika mchakato wa usuluhishwaji wa malalamishi. Haihitajiki kuwa na wakili, na unaweza kufanikiwa bila hata ya wakili. Mara kwa mara ni vyema kupata ushauri wa wakili ama mtu mwingine mwenye uelewa ili kusaidia kutuma ombi na kuandaa kwa kusikilizwa kwa malalamishi.
Nitaomba mchakato wa usikilizwaji wa malalamishi?
Tuma ombi kwa maandishi kwa Office of Administrative Hearings (Ofisi ya Usikilizwaji wa Malalamishi) na fahamisha wilaya ya shule.
Ombi na mchakato wa kusikilizwa kwa malalamishi na lifanywe kwa maandishi na lina taarifa ifuatayo:
- Jina na anwani ya mwanafunzi
- Wilaya na shule mwanafunzi anahudhuria
- Wilaya inayohusika kwa kutoa huduma maalum ya elimu iwapo ni tofauti kutoka kwa wilaya ambayo mwanafunzi anaposomea
- Maelezo ya hofu ya kuhusu wazazi
- Mapendekezo yako ya kutatua matatizo.
Tuma barua ama kufikisha nakala ya ombi la malalamishi kwa:
Office of Administrative Hearings
P.O. Box 42489
Olympia, WA 98504
Kadhalika, unapaswa kutoa ombi la malalamishi halisi kwa wilaya ya shule kwa kufikisha ama kutuma barua kwa Msimamizi wa Wilaya ya Shule. Usisahau kijiwekea nakala!
OSPI iliunda ombi la fomu ya mchakato wa kusikiliza malalamishi ili kusaidia mzazi kuomba mchakato wa kusikilizwa kwa malalamishi. Fomu hii inapatikana kupitia: https://ospi.k12.wa.us/student-success/special- education/dispute-resolution/request-due-process-hearing
Ni viwango vipi vya ombi la mchakato wa kusikiliza malalamishi?
Ombi la mchakato wa kusikilizwa kwa malalamishi lazima lishughulikie ukiukaji ama tatizo lililotokea ndani ya miaka miwili iliyopita. Ombi la mchakato la kusikiliza malalamishi linafaa kushughulikia ukiukaji kutoka kwa zaidi miaka miwili iliyopita iwapo masharti mawili yameshughulikiwa:
- Mzazi alizuiwa kuomba kuhusu mchakato wa kusikilizwa kwa malalamishi ndani ya miaka miwili kwa sababu wilaya ya shule haikuwakilisha vyema kwamba ilitatua tatizo hilo
Au
- Mzazi alizuiwa kuomba kuhusu mchakato wa kusikilizwa kwa malalamishi ndani ya miaka miwili kwa sababu wilaya ya shule ilizuia taarifa iliyohitajika kutoa kisheria.
Ni muhimu sana kusikiliza ombi ili kujadili matatizo yote na hofu aliyokonayo mzazi. Baada ya ombi kupokelewa, linaweza tu kubadilishwa iwapo wilaya ya shule itakubali kwa maandiko ama ikiwa ofisa wa kusikiliza malalamishi atakapokubali kwamba inaweza kubadilishwa, na kipindi cha muda wa usuluhishaji (tazama hapo chini) kuanza upya.
Kadhalika, chini ya IDEA, masuala yaliyojadiliwa katika ombi la usuluhishwaji ama katika mabadiliko kwa ombi linaweza kushughulikwa labda pengine wahusika wa upande mwingine wakubali. Huku ukiwa huhitajiki kuwa na wakili ili kutuma ombi la kusikilizwa kwa malalamishi, inaweza kusaidia kuwasiliana na wakili wakati wa kuandika ombi la kusikilizwa kwa malalamishi, ili kuhakikisha kwamba wasiwasi wako umezungumziwa.
Itakuwaje baada ya kutuma ombi la kusikilizwa kwa malalamishi?
Wilaya ya shule lazima ijibu.
Ndani ya siku 10 baada ya kupokea malalamishi, wilaya ya shule lazima ijibu. Ni lazima wilaya ya shule ielezee ni kwa nini ilichukua hatua iliyochukua, ni machaguo yapi mengine Timu ya IEP ilipendekeza na ni kwa nini ilikataliwa, maelezo ya taarifa ambayo wilaya ilitegemea na kufanya maamuzi yake na taarifa katika masuala mengine kwa maamuzi ya wilaya. Wilaya ya shule haihitaji kujibu iwapo ilituma ilani kwa maandiko kwa mzazi kuhusu suala husika katika malalamishi.
Je, kipindi cha usuluhishaji ni nini?
Kipindi cha usuluhishaji ni kikao kinachofanyika baada ya ombi la usikilizwaji wa malalamishi umefanyika, lakini kabla ya kusikilizwa kwa malalamishi.
Ndani ya siku 15 za kupokea ombi la kusikilizwa kwa malalamishi kutoka kwa mzazi, wilaya ya shule lazima paitishwe kikao na mzazi, wanachama wahusika wa Timu ya IEP, na wawakilishi wa wilaya ya shule ambayo mamlaka ya kufanya maamuzi. Wilaya ya shule haiwezi kuleta wakili kwa mkutano huo mpaka mzazi awe na wakili pia. Lengo la kikao hiki ni kujadili malalamishi na kuona iwapo tatizo linaweza kutatuliwa bila ya mchakato wa kusikilizwa kwa malalamishi.
Iwapo mzazi na wilaya ya shule wataelewana katika kipindi cha suluhisho, basi ni lazima watie sahihi makubaliano ya kisheria yanayofikia viwango vya kufikishwa kortini. Vile vile wilaya ya shule ama mzazi ana siku tatu za biashara kubadilisha mawazo yao na kubatilisha makubaliano.
Kipindi cha makubaliano ni lazima kifanyike mpaka pale ambapo mzazi na wilaya ya shule watakubaliana kwa maandiko ili kubadilisha mkutano au badala yake kukubaliana kutumia upatanishi.
Je, usikilizwaji wa utaratibu huo utachukua muda gani?
Wilaya ya shule ina siku 30 kutoka wakati ambapo inapopokea malalamishi ili kujaribu kutatua tatizo kwa kutosheka kwa wazazi kupitia kwa utaratibu wa upatanishi. Iwapo wilaya haitafanya hivyo ndani ya siku 30, kisha muda wa kusikilizwa unaanza. Usikilizwaji unapaswa kufanywa na maamuzi kufikiwa ndani ya siku 45.
Upatanishi wa siku 30 hubadilishwa iwapo tu baadhi ya mambo yafuatayo yatatokea:
- Pande zote mbili zikubaliane kwa maandiko ili kupunguza kipindi cha suluhisho.
- Baada ya kipindi cha upatanisho ama suluhu, pande zote zikubaliane kwa maandiko kwamba hakuna makubaliano yatakayowezekana ama
- Pande zote zikubaliane kushiriki katika upatanisho nje ya kipindi cha upatanisho cha siku 30 na chama kimoja kitaondoka kutoka kwenye upatanisho Katika hali hizi, muda wa siku 45 unaanza mara moja.
Urefu wa kipindi chenyewe cha usikilizwaji kitategemea pakubwa matatizo yaliyopo na ni kwa muda gani kila upande utachukua ili kusikilizwa kwa malalamishi hayo.
Kipindi cha upatanishi ni muhimu sana. Iwapo mzazi hataki kushiriki katika kipindi cha utafutaji suluhu, muda wa kikao cha usuluhishaji na utaratibu wa kusikilizwa utacheleweshwa mpaka kikao kitakapofanyika. Zaidi ya hayo, wilaya ya shule inaweza kuuliza tena afisa wa usuluhisho baada ya kukamilika kwa kipindi cha suluhu cha siku 30 ili kujadili utaratibu wa ombi la usulihishaji iwapo mzazi atakataa kushiriki kwenye kikao cha usuluhishaji.
Kwa upande mwingine, iwapo wilaya ya shule itafeli kuandaa kikao cha usuluhishaji ndani ya siku 15 baada ya kupokea ombi hilo, mzazi anaweza kumuuliza ofisa wa usuluhishaji ili mara moja kuanza mchakato wa siku 45 za kipindi cha usikilizwaji wa malalamishi.
Kipindi cha Mchakato wa Kusikilizwa kwa Malalamishi
Ombi la mzazi la kusikilizwa kwa maandiko |
Wilaya inajibu ndani ya siku 10 |
Ratiba ya kipindi cha suluhisho cha Wilaya ndani ya siku 15, hadi pale itakapoondolewa kwa maandiko |
Iwapo kipindi cha usuluhishaji, hakitatatua malalamishi ndani ya siku 30, utaratibu wa usikilizwaji utaendelea na maamuzi ya yatafanywa ndani ya siku 45 |
Ni nini maana ya “kunyamaza?” Mwanafunzi wangu ataenda shule gani nitakapoomba kusikilizwa kwa malalamishi?
Nyamaza ni neno linalotumika katika IDEA ili kuelezea kule mtoto anaposomea pale usikilizwaji utakapoitishwa. Iwapo usikilizwaji utaitishwa, mwanafunzi ana haki kuendelea kupokea programu yao binafsi ya kielimu katika mpangilio sawa hadi pale ambapo usikilizwaji utakapokamilika na maamuzi kutolewa. Kuna baadhi ya masuala ya kunyamazia inayotumika wakati wanafunzi walio na ulemavu wanapotiwa nidhamu.
Je, usikilizwaji wa kiutaratibu unaweza kufanikiwa kivipi kwa mwanafunzi wangu?
Wilaya inaweza kushurutishwa kutoa huduma, kumpatia mwanafunzi elimu ya fidia, na kulipia ada ya uwakilishwaji kisheria.
Usikilizwaji wa kiutaratibu unaweza kusaidia kupata huduma zinazofaa na kufidia elimu ambayo haikutolewa na wilaya. Ofisa wa Usikilizaji anaweza kutatua migogoro kuhusu ustahiki wa mwanafunzi, IEP, mabadiliko ya mipangilio ya kielemu, na utathmini na utathmini upya.
Ofisa wa Usikilizaji pia anaweza kuagiza elimu ya fidia, ikimaanisha wilaya lazima itoe huduma ili kufidia muda ama fursa zilizokosekana kwa sababu ya kufeli kwa wilaya. Kwa mfano, wilaya inaweza kuamrishwa kulipia mwanafunzi ili kushiriki katika kozi ya asasi ya kijamii, kutoa mafunzo ili kuongezea programu ya elimu maalum, ama wezesha programu za majira ya joto, hata kama mwanafunzi hatafikia vigezo vya huduma za mwaka wa shule ulioongezewa.
Ni lazima maombi ya fidia ya elimu yahusiane na malengo na majukumu ya IEP. Kuwa mbunifu unapoulizia kuhusu huduma za fidia ya elimu. Fikiria kuhusu kile ambacho mwanafunzi anapenda kufanya (sanaa, muziki, sayansi, n.k) na pendekeza programu ama huduma inayotua maarifa haya.
Iwapo utashinda katika usikilizwaji, wilaya inaweza kuhitajika kulipia gharama uliyotumia wakati wa usikilizwaji na ada alizotoza wakili ili kumuwakilisha. Weka rekodi ya gharama uliyotumia kwenye maandalizi ya kusikilizwa kwa malalamishi haya.